Wakati Wafanyakazi Duniani kote wakiadhimisha siku yao (Mei Mosi), Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewaagiza waajiri kuhakikisha zawadi kwa Wafanyakazi hodari zinapatikana kwa wakati na si vinginevyo.
Gondwe ametoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani kiwilaya yaliyofanyika kwenye viwanja vya soko la zamani Chanika ambapo yeye amealikwa kama mgeni rasmi.
"Kumekuwepo na malalamiko mengi toka kwa watumishi hodari kwa kipindi cha miaka ya nyuma kutopewa zawadi zao mpaka wanakata tamaa sasa nawaagiza waajiri kutoka Halmashauri zote mbili yaani Wilaya na Mji kuwapa stahiki zao kwa wakati na ninaahidi mbele ya maadhimisho haya nitafuatilia suala hili kwa karibu zaidi"
Kuhusu Watumishi kupandishwa vyeo na nyongeza ya mishahara, Gondwe amesema kwa upande wa Halmashauri ya Mji Handeni Serikali imetenga jumla ya nafasi 383 za watumishi kupandishwa vyeo, kwa hiyo watumishi wasiwe na wasiwasi waendelea kufanya kazi kwa bidii kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kauli mbiu yake ya hapa kazi tu.
Akizungumzia agizo hilo, Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Thomas Mzinga amesema Ofisi yake itahakikisha kabla ya tarehe 05/05/2018 kila Mfanyakazi hodari atakuwa amepatiwa zawadi yake kama ilivyotangazwa.
Pichani:Mfanyakazi hodari toka Halmashauri ya Mji Handeni Bi.Grace Gambadu akipongezwa na Watumishi wenzake kwenye maadhimisho ya Mei Mosi
pichani:Mfanyakazi hodari bw.Hassan Mhina akipongezwa na Watumishi wenzake kwenye maadhimisho ya Mei Mosi
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.