Ziara ya Mkuu Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila Kata za Kwenjugo na Mdoe Tarehe 01/10/2020.
Mkuu wa Wilaya amefanya ziara ya kawaida katika Kata hizo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, katika ziara hiyo ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya pamoja Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni bw.Kenneth Haule na Wataalam wake.
Kero kubwa zilizojitokeza ni migogogro ya Ardhi, upatikanaji wa Maji, ukosefu wa Zahanati Kata ya Kwenjugo, umeme, Akitolea ufafanuzi kero hizo DC amesema suala la Zahanati ya Kwenjugo yupo tayari kuhakikisha inajengwa na kwa kuanzia amesema anataka kushirikim msalagambo wa kuchimba Msingi kwa kushirikiana na wananchi na pia atatoa gari kwa ajili ya kusomba mchanga na mawe.
Migogoro ya Ardhi imeonekana wananchi wanahitaji kuendelea kupatiwa Elimu juu sheria zinazohusu umiliki wa ardhi, katika hatua nyingine ameamuru wananchi walionyanganywa mashamba yao bila kufuata taratibu warudishiwe mara moja .
Kuhusu tatizo la Maji DC amesema kuanzia mwakani tatizo la Maji Handeni litakuwa historia kwa sababu serikali kupitia mradi wa HTM imeweka zaidi ya Tshs.300 ili kuukarabati upya mradi huo ambapo maji yatapatikana kwa wingi maeneo yote ya Halmashauri ya Mji Handeni.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.