Malengo ya uanzishwaji wa Programu(MUP)
Malengo ya programu ni kuwezesha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya awali na msingi Tanzania Bara. BOOST ni sehemu ya mpango wa Lipa kutokana na matokeo katika Elimu awamu ya pili(EPforR II) na inachangia katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa sekta ya elimu wa miaka mitano 2021/22 hadi 2025/26
Matokeo muhimu
Vyumba vipya vya madarasa 12,000 kujengwa na vifaa vya shule vinavyohusika katika maeneo yenye uhitaji zaidi
Vituo 800 katika shule za msingi /vituo vya walimu kuanzishwa na kuendelezwa kwa ajili ya utoaji wa mafunzo kwa njia ya TEHAMA kupitia maktaba mtandao/kielektroniki na mfumo wa usimamizi wa ujifunzaji kimtandao
Shule za msingi 6,000 kuwezeshwa kutekeleza programu ya shule ya msingi salama.
Madarasa 12,000 ya elimu ya awali yaliyoboreshwa pamoja na njia bora za ufundishaji vikiwemo vifaa vya ujifunzaji
Kuongezeka kwa uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali kutoka asilimia 76.9 hadi asilimia 85.
Kuongezeka kwa uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali kutoka asilimia 57.5 hadi asilimia 65.6 kwa Halmashauri zilizo katika kundi la robo ya chini
Kuongezeka kwa kiwango cha wanafunzi kubaki shuleni kwa Halmashauri zilizo katika kundi la robo ya chini kutoka asilimia 55.9 hadi asilimia 66.24
Asilimia 50 ya wanafunzi wa darasa la pili kufikia kiwango cha chini cha kumudu stadi za kusoma na kuandika na asilimia 35 katika kuhesabu
Ushiriki wa walimu katika mpango wa mafunzo Endelevu ya walimu kazini (MEWAKA) kufikia asilimia 50
Kuimarisha mfumo katika:
Takwimu, mipango, ufuatiliaji na tathimini ya maendeleo ya sera yanayotokana na ushahidi
Maendeleo ya sera yanayotokana na uthibitisho
Ujenzi wa miundombinu kwa kushirikisha jamii
Uwezo wa kitaifa katika uandaaji wa mitaala na upimaji katika ujifunzaji
Umahiri wa matumizi ya TEHAMA kwa wanafunzi na walimu wa shule za msingi
Mfumo wa kitaifa wa mafunzo endelevu ya walimu kazini(MEWAKA)
Kuimarisha maktaba mtandao na mfumo wa usimamizi katika ujifunzaji
Halmashauri zinazozingatia utawala bora katika elimu
Maendeleo ya elimu yanayozingatia mazingira na hali za jamii
Hii ndio programu ya BOOST, ambayo hivi leo Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Mwalimu Newaho Mkisi amefungua mafunzo ya siku mbili kwa watumishi 234 wa kada teule kutoka Halmashauri 18 za mikoa ya Kilimanjaro na Tanga, watumishi wa ofisi za wadhibiti ubora elimu, watumishi wa ofisi za TSC na wale wa sekretarieti za mikoa, yatakayofanyika katika Ukumbi wa Shule ya wasichana Korogwe mkoani Tanga, yakiwa na shabaha ya kuwajengea uwelewa wa programu ya BOOST na uwezo kabambe wa kwenda kutekeleza malengo ya programu hiyo.
Mratibu msaidizi wa programu ya BOOST kitaifa kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Ndugu. Reuben Swilla akizungumza mbele ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo watumishi kuhusu program ya BOOST.
Afisa Elimu Mkoa wa Tanga na Mgeni rasmi Mwalimu Newaho Mkisi katika ufunguzi wa mafunzo ya program ya BOOST kwa watumishi wa Halmashauri na Sekretarieti za mikoa ya Tanga na Kilimanjaro akizungumza na washiriki.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, mgeni rasmi na Afisa Elimu mkoa wa Tanga amewasihi sana washiriki wa mafunzo hayo, kuzingatia weledi, ushirikiano wa hali ya juu miongoni mwao watakaporudi kutekeleza malengo ya programu katika maeneo yao.
Washiriki wa mafunzo ya programu ya BOOST wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku mbili
Mwandishi wetu
Handeni mji
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.