Kwa watoto wote
Mradi wa Shule Bora umelenga kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wote wa kike na wa kiume katika shule za Serikali za Tanzania.
Kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania mradi huu utafanya maboresho yatakayowezesha kila mtoto kupata msingi mzuri katika elimu yake ya awali, ili kuitumia fursa kwa kutoa mchango wake katika ukuaji wa nchi na maendeleo yake.
Changamoto zitakaposhughulikia
Wakati watoto wengi wakijiunga na kuendelea na masomo, matokeo ya elimu Tanzania yamekuwa na changamoto nyingi. Ni asilimia nane tu (8%) ya wanafunzi katika elimu ya msingi wanafikia kiwango cha Taifa cha kujua kusoma kwa ufasaha, 12% wanafikia kiwango cha Taifa cha kuwa na ujuzi wa kujumlisha na kutoa.
Kwa kiasi fulani hii inachangiwa na ongezeko la uhitaji wa elimu msingi sambamba na ongezeko la idadi ya watu kunakopelekea ongezeko la uwiano wa walimu na wanafunzi, ambako kwa sasa ni wastani wa wanafunzi sitini na mbili kwa kila mwalimu mmoja kwa shule za msingi za Serikali.
Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Mwl.Ewapo Mkisi akizungumza na waandishi wa habari siku ya mafunzo juu ya programu ya shule bora katika ukumbi wa Korogwe Executive, Tanga.
Unalenga matokeo
Katika ngazi ya kitaifa Shule Bora itatoa msaada wa kiufundi kwa Serikali ya Tanzania, pamoja na utekelezaji wa mradi wa wafadhili wa lipwa kwa matokeo yaani Education Program for Result II (EPforRII).
Malengo ya utekelezaji wa kitaifa kuwa yanapangwa kwa pamoja kati ya Serikali na wafadhili huku utoaji wa fedha ukihusisha malengo yaliyofikiwa. Hii inasisimua mabadiliko ya kimfumo kama yale ya msawazo sawa wa walimu na ugawaji wa vitabu.
Shule Bora pia itafadhili matokeo muhimu yatakayotokana na vigezo vilivyothibitishwa toka katika mradi wa EPforR ambavyo vitatumika katika utoaji wa fedha na wafadhili wengine.
Kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid, gharama za mradi zitakuwa na bajeti ya paundi za kiingereza 89 millioni, sawa na shilingi za kitanzania bilioni 271 na utafanya kazi katika ngazi zote za mradi. Mradi huu wa Shule Bora utatekelezwa hadi ifikapo mwaka 2027.
Ushirikiano na ubunifu
Shule bora itafanya kazi moja kwa moja na mamlaka za Serikali za Mikoa na Halmashauri pamoja na shule katika Mikoa tisa yenye changamoto nyingi kama ilivyopendekezwa na kukubalika na Serikali ya Tanzania; katika kuboresha elimu. Inakadiriwa kuwa mradi huu utawafikia watoto takribani Milioni Nne wa kitanzania, kati yao nusu ni wasichana.
Mabadiliko ya ubunifu yataonekana na kutathminiwa katika ngazi za chini ambazo walengwa muhimu watapatikana katika shule zote za msingi Tanzania.
Shule bora inalenga katika mambo manne;
1
|
Kujifunza
|
Watoto wote wanajifunza katika shule.
|
2
|
Kufundisha
|
Mfuko wa msaada wa UK utaunga mkono na kuimarisha kazi ya ufundishaji Tanzania.
|
3
|
Jumuishi
|
Kuhakikisha kuwa watoto wote wa kitanzania mashuleni wanakuwa katika mazingira salama na rafiki ili kuwawezesha kumaliza elimu ya msingi na wanaendelea na elimu ya Sekondari;na
|
4
|
Kujenga mfumo
|
Mfuko wa UK Aids utaunga mkono Serikali na kuimarisha ili kupata au kuwa na thamani ya fedha katika utoaji wa elimu katika ngazi zote toka chini hadi Tifani.
|
Mikoa ambayo Programu ya shule bora inatekelezwa
Jumuishi ni kipaumbele cha Shule Bora
Mradi utawatupia macho kwa karibu wanafunzi wa kike, wanafunzi wenye mahitaji maalum na wale wanaotoka katika mazingira magumu. Mradi pia utashughulikia mambo yatakayowezesha watoto kuwa shuleni katika mazingira bora na salama ili kuwapa nafasi ya kujifunza na kuendelea na masomo yao ya Sekondari.
Hii ni pamoja na kuwashirikisha wazazi na jumuiya katika kuboresha usalama wa shule na kuondoa migogoro,kuhakikisha kuwa walimu wanazungumzia mambo ya jinsia na upatikanaji wa mahitaji ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu.
Pia kutayarisha mazingira salama na kuwaunga mkono wasichana kushiriki pamoja na kujadili mambo yanayowahusu pamoja na kuwasaidia katika kipindi cha hedhi.
Mradi wa Shule Bora utaisaidia Tanzania kutengeneza mfumo wa elimu utakaofanana na wa UK ambao utawezesha kuondoka(kuziba) pengo kati ya wasichana na wavulana kwa kiasi kikubwa na kwa maeneo mengi wasichana kwa sasa wanalingana na wavulana katika kujiunga elimu ya msingi,viwango vya kusoma na kuandika pia.
Na uzuri zaidi idadi ya wasichana wanaohitimu elimu ya msingi na sekondari inaizidi ile ya wavulana.
Mipango ya mfuko wa UK aids pia imeimarisha ubora wa elimu na mafunzo kwa watoto wapatao milioni 3.1
Tathmini iliyofanywa ilionekana kuwa juhudi za mfuko wa UK aids zilichangia ongezeko la watoto takribani mara mbili Zaidi kuliko wale ambao walikuwa nje ya jitihada za mfuko huo.
Mpango kazi wa kwanza wa utekelezaji wa mradi wa Shule Bora baada ya uzinduzi utajumuisha jitihada zitakazopelekea;
Mradi wa Shule Bora ni zao la mfuko wa UKAID kwa Serikali ya Tanzania ikilenga kuunga mkono miradi ya elimu Tanzania. Unatekelezwa katika Mikoa tisa ya Tanzania kwa kupokea utaalamu wa kiufundi toka Cambridge Education ikishirikiana na mashirika ya ADD International, International Rescue Committee na Plan International.
Kwa taarifa Zaidi; www.camb-ed.com au barua pepe:CETanzania@camb-ed.com, na simu: +255 759957880
Handeni Mji
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.