Mtandao wa simu za mkononi Tigo umezindua mradi wa eSchool katika Shule ya Sekondari Handeni iliyopo katika Halmashauri ya Mji Handeni.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela,Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Mkoa amesema" kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imekuwa ni rafiki mzuri wa Serikali na imejikita sana katika shughuli za maendeleo ya Jamii".Mradi wa huu wa Kieletroniki unasaidia kusambaza stadi za kisasa za TEHAMA pamoja na uelewa kwa vijana na kuwawezesha kukabiliana na changamoto zinazotokana na mtririko wa mabadiliko ya habari ya kila siku ndani ya Jamii na katika uchumi wa Dunia.
Vilevile mradi huu unawawezesha Vijana na Jamii kwa ujumla kuingia katika mkondo wa kidunia wa Habari na uelewa,ambako watajifunza kupanua uelewa wao na kushirikiana na wenzao katika sehemu mbalimbali Duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela akizindua mradi wa Tigo eSchool katika Shule ya Sekondari Handeni
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe.Godwin Gondwe akizungumza kwenye uzinduzi Tigo eSchool Shule ya Sekondari Handeni
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Handeni wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa Tigo eSchool shuleni hapo
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.