Katika jitihada za kukabiliana na uhaba wa vyumba vya Madarasa katika Halmashauri ya Mji handeni juhudi mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kutatua changamoto hiyo..
Ofisi ya Mkurugenzi kwa kushirikiana na Wananchi wa Kata ya Chanika leo tarehe 29/12/2018 imeongoza "msalagambo" wa kuchimba msingi wa ujenzi wa vyumba vinne (4) vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kivesa ambapo kwa umoja wao zoezi hilo limefanyika kwa mafanikio makubwa.
Katika zoezi hilo Wananchi wa Kata ya Chanika wameongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe.Chihumpu na kwa upande wa Ofisi ya Mkurugenzi watumishi wameongozwa na kaimu Mkurugenzi Bw.Thomas mzinga
Wananchi waliojitokeza kwenye zoezi la kuchimba msingi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kivesa wakiendelea kuwajibika hapo juu kwenye picha
Halmashauri imejipanga kuhakikisha watoto wote waliofaulu darasa la saba wanajiunga na kidato cha kwanza kuanzia mwaka wa masomo 2019. Mbali na zoezi la leo la kuchimba msingi vile vile Halmashauri inaendelea na zoezi la kukusanya michango ya fedha tasilimu kutoka kwa wadau mbali mbali wa Elimu.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.