Siku ya kufanya Usafi wa mazingira Halmashauri ya Mji Handeni imeadhimishwa kwa Watumishi wake kusafisha eneo la dampo Kwenjugo.
Zoezi la Usafi wa mazingira hufanyika kila jumamosi ya mwisho ya kila mwezi ambapo kwa Mwezi huu Halmashauri imeshiriki kwa kufanya usafi eneo la dampo lililopo katika Kata ya Kwenjugo,Watumishi wa makao makuu wakishirikiana na viongozi wa Kata za Mdoe, Chanika, Kwenjugo na Vibaoni wamejitokeza kwa wingi kusafisha eneo hilo.
Usafi uliofanyika eneo hilo ni kukusanya taka zilizosambaa eneo la dampo na kuzichoma pamoja na kusogeza taka zilizo karibu na bararbara.Wakizungumza wakati wa zoezi hilo Watumishi hao wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw.Thomas Mzinga wameshauri eneo hilo kuwekewa uzio ili kuzuia watu wasiowaaminifu kutupa taka hovyo eneo hilo kwa sababu imeonekana watu hawafuati taratibu za matumizi ya dampo.
Mmoja wa watu waliojitokeza akishiriki Usafi
Afisa Elimu Msingi Bw.Omari Mashaka na Mdhibiti ubora Elimu Bi.Donesia Mwalukasa wakishiriki zoezi la Usafi
Afisa Elimu Kata ya Chanika Bi.Oliver Mmbaga akishiriki zoezi la Usafi
Afisa Michezo Bi.Mawazo Mohamedi akishiriki zoezi hilo eneo la dampo
Bw,Mongela Semhale muangalizi wa Ofisi akishiriki zoezi la Usafi eneo la dampo
Watumishi waliojitikeza wakiendelea na zoezi la Usafi eneo la dampo
Afisa Taaluma Sekondari Bi,Elizabeth Kitururu akichoma taka wakati hilo
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.