Katika kikao cha madiwani cha tarehe 28/4/2023, moja ya Agenda waliyokubaliana ni kupita kwenye nyumba za ibada na kuhamasisha na kuelezea namna ambayo maadili yamepotea kwenye jamii yetu. Katika kufanikisha hili leo tarehe 14/05/2023 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni Mhe Musa Mkombati (Diwani), aliendelea na ziara yake kwenye makanisa ya Kideleko, Kwaluwala, Kwamgome, Majeshi majeshi na E.A.G.T -Kwamngumi. Kwenye ziara hiyo Mhe Diwani aliongozana na Bi Amina Waziri (Afisa Maendeleo ya Jamii) kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni.
Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni amewataka viongozi wa dini kushirikiana na wazazi, walezi pamoja na walimu kuwaongoza katika kupambana na janga hili, vilevile aliwaeleza kuwa “mmomonyoko wa maadili hasa vitendo vya ushoga, ndoa za utotoni pamoja na mapenzi ya jinsia moja vinafadhiliwa na watu wenye nguvu za kifedha, hivyo basi mtu mmoja mmoja hawezi kupambana nao ndio maana tumeamua kutumia viongozi wa dini katika vita hii”. Wakati huohuo amewashauri wazazi kuwa makini na ndugu wa karibu wanapokuja kutembelea nyumbani, maana matendo mengi ya ubakaji yanatokea kwa watu wa karibu, hivyo basi aliwataka wageni wasiachwe kulala na watoto kwenye chumba kimoja.
Pia amewaambia watoto wakatae na watoe taarifa kwa walimu, wazazi na viongozi wa dini pindi wanapofanyiwa matendo ya unyanyasaji.
Alimalizia kwa kusema Handeni bila Ndoa za Utotoni, ushoga na ndoa za jinsia moja inawezekana
Mwenyekiti wa Halmasahuri Mhe.Musa Mkombati (Diwani) akizungumza na waumini katika Kanisa la Majeshi Majeshi juu ya mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Amina Waziri, aliwaasa waumini kulea watoto kwenye misingi ya mtoto wa mwezako ni wako, na sio kama ilivyo sasa kusema ”Asiyefunzwa na mamae atafunzwa na ulimwengu” tuachane na maneno au dhana hiyo, kwa nguvu za pamoja tunaweza kuondoa janga hili.
Pia aliwaasa wazazi kuzungumza na watoto wao mara kwa mara kujua matatizo yao na sio kujishughulisha na kazi pamoja na kutafuta pesa
Bi Amina Waziri (Afisa Maendeleo ya Jamii) akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyeketi wa Halmashauri kuja kuongea na waumini wa Kanisa la Kideleko kushoto ni mwenyeji wake diwani wa kata ya Kideleko Mhe.Godfrey Munga
Pia Padre William Mkeni wa Kanisa la Kideleko, ameshukuru jitihada zinazofanywa na serikali na kuahidi kuunga mkono juhudi hizo, zenye tija katika kuimarisha maadili mema katika jamii. Alihitimisha kwa kuwakumbusha waumini kwa kusema “Mungu alisema nendeni mkajaze ulimwengu sio kwa ndoa za jinsia moja bali ni kwa mke na mume”.
Padre William Mkeni wa Kanisa la Kideleko akitoa neno la shukurai kwa mgeni rasmi
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.