Leo tarehe 13 Januari 2023 ikiwa ndiyo siku ya mwisho ya utekelezaji wa agizo la Serikali kuhusu ugawaji wa vishikwambi kwa walimu, waratibu Elimu kata na maafisa Elimu ngazi ya Halmashauri, Halmashauri ya Mji Handeni ilipokea jumla ya vishikwambi 319 vilivyotumika katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na imegawa vishikwambi vyote 319 kwa mchanganuo ufuatao vishikwambi vitatu(3) wamepatiwa maafisa elimu ngazi ya Halmashauri, vishikwambi kumi na mbili(12) wamepatiwa waratibu Elimu kata na vishikwambi 304 wamepatiwa walimu wa shule za msingi na sekondari. Hata hivyo jumla ya idadi ya walimu wote katika Halmashauri ya Mji Handeni ni 588 ikiwa waliopata vishikwambi ni 304 sawa na asilimia 51.7 na upungufu ukiwa ni vishikwambi 284 sawa na asilimia 48.3 ya walimu wote ambao hawajapata vishikwambi.
Akizungumza wakati wa kupokea vishikwambi hivyo Mwalimu Goefrey William Daiford kutoka shule ya Sekondari Kileleni amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha sekta ya Elimu Nchini ambapo kutokana na vishikwambi changamoto mbalimbali zinakwenda kutatuliwa ikiwemo kupata dhana tofauti kutoka mtandaoni na kuweza kutunza kumbukumbu katika vishikwambi na hivyo kuongeza ufanisi kwenye kutoa Elimu wakati huohuo amewaahidi wazazi na walezi wategemee wanafunzi kupata Elimu iliyo bora na ya kisasa kwani kuwepo kwa vishikwambi kutaongeza ubora wa Elimu inayotolewa.
Mwalimu Goefrey William Daiford(kulia) akipokea vishikwambi kutoka kwa Afisa Elimu Sekondari vifaa na takwimu Bw Montan Mathew(kushoto).
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi. Maryam Ukwaju amewasisitiza walimu kuzingatia utaratibu uliowekwa juu ya matumizi sahihi ya vishikwambi kama ifuatavyo:-
Na mwandishi wetu
Handeni Mji
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.